KOCHA EMMANUEL AMUNIKE AITA WACHEZAJI 30 TAIFA STARS KUIKABILI CAPE VERDE

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini Septemba 30 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Africa dhidi ya Cape Verde.

Katika kikosi hicho kinachodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager Kocha Amunike amewaongeza wachezaji watano (5) kutoka kwenye kikosi cha awali.

Wachezaji walioongezwa ni Jonas Mkude,Shomari Kapombe, John Boko (Simba),Feisal Salum(Young Africans) na Abdallah Kheri (Azam FC).

Kikosi kilichoitwa.

Aishi Manula (Simba)
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Frank Domayo(Azam FC)
Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC)
Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Young Africans)
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Andrew Vicent (Young Africans )
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya zaydi(Azam FC)
Kelvin Yondan (Young Africans)
Paul Ngalema (Lipuli)
Jonas Mkude (Simba)
John Boko (Simba)
Shomari Kapombe (Simba)
Feisal Salum (Young Africans)
Abdallah Kheri (Azam FC)

kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Makocha wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi,Mtunza Vifaa Ally Ruvu na madaktari Richard Yomba na Gilbert Kigadya.